MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 6 AFARIKI DUNIA KWA KUSHAMBULIWA NA FISI SHINYANGA MJINI

Picha ya fisi
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtoto aitwaye Kulwa Machiya (06) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kung’atwa na fisi sehemu za usoni katika eneo la Relini - Nhelegani Mjini Shinyanga. 

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokea Agosti 1,2020 majira ya saa 12 jioni wakati mtoto huyo akiwa njiani kurudi nyumbani akitokea kuchunga ng’ombe akiwa na watoto wenzake. 

“Mtoto wa kiume aitwaye Kulwa Machia mwenye umri wa miaka 6,mkazi wa eneo la Relini- Nhelegani tarafa ya Shinyanga Mjini alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kung'atwa na fisi sehemu za usoni na kusababishiwa majeraha makubwa usoni wakati akiwa njiani kurudi nyumbani akitokea kuchunga akiwa pamoja na watoto wenzake kisha fisi huyo kutokemea vichakani baada ya kusikia mayowe ya watoto hao waliokuwa na marehemu”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Kamanda Magiligimba amesema elimu ya kujinga na wanyama wakali imetolewa  na anatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao kwani kipindi hiki yameripotiwa matukio mengi ya kuwajeruhi na kuwaua watoto walio na umri chini ya miaka 10 mkoani Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post