TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI - NEC YATANGAZA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU TANZANIA KUANZA AGOSTI 26,2020



Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage akizungumza jambo na Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh.Asina Omary wakati wa ufunguzi wa kikao kati ya NEC na vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage akizungumza leo Agosti 1,2020 katika ufunguzi wa kikao kati ya NEC na vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar,ambapo Kaijage pia alitangaza kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu,kwamba zitaanza Agosti 26 mwaka huu na kumalizika Oktoba 28 ,2020 kwa upande wa Tanzania Bara.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt Wilson Mahera akionesha moja ya kijarida chenye maelekezo mbalimbali kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt Wilson Mahera akifafanua jambo mbele ya Viongozi wa vyama vya siasa mbalimbali wakati wa ufunguzi wa kikao kati ya NEC na vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wawawikilishi wa vyama vya siasa wakiwasilisha hoja zao mbalimbali mbele ya viongozi wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa kikao. 



Baadhi ya Wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye kikao hicho .

***
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TUME ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu(NEC) imetangaza kuwa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu zitaanza Agosti 26 mwaka huu na kumalizika Oktoba 28 ,2020 kwa upande wa Tanzania Bara.

Akizungumza leo Agosti 1,2020 katika ufunguzi wa kikao kati ya NEC na vyama vya siasa kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage pia amesema kwa kuzingatia ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Tume ya Taifa Zanzibar(ZEC) kampeni za uchaguzi kwa Zanzibar zitaisha Oktoba 26,2020 ili kupisha upigaji kura ya mapema ya Rais wa Zanzibar,mwakilishi na diwani.
 
Amevitaka vyama vya siasa kupanga ratiba zao za kampeni ambazo zitaisha Oktoba 26 mwaka 2020 kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Hata hivyo amefafanua kuwa kama ambavyo imeripotiwa kupitia vyombo mbalimbali ,NEC tayari imetoa ratiba ya uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani na kama amnavyo wamesikia uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika siku ya Jumatano ya Oktoba 28 mwaka huu na tayari Serikali imetoa tamko kupitia gazeti la Serikali namba 578 la Julai 24,2020 ambayo siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko.

"Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fomu za uteuzi zitaanza kutolewa Agosti 5,2020 kwenye makao makuu ya NEC jijini Dodoma kwa wagombea wa kiti cha Urais.Fomu kwa ajili ya ubunge na udiwani zitatolewa kwenye makao makuu ya hamashauri yaliyopo majimbo na kata husika kuanzia Agosti 12 hadi Agosti 25 ,2020,amesema Jji mstaafu Kaijage.

Aisha urejeshaji wa fomu utafanyika Agosti 25 mwaka huu kabla ya saa 10 kamili jioni ambayo ndio siku ya uteuzi."Naomba kutoa rai kwenu kuzingatia ratiba hiyo na kuwasisitiza wagombea kutoka katika vyama vyenu kujaza fomu kwa usahihi ili kuepuka dosari zinazoweza kuwafanya kushindwa kuteuliwa

"Kayla kipindi cha uteuzi ,wagombea pia wana haki ya kisheria na kuweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.Aidha Mkurugenzi wa Uchaguzi ,mwanasheria mkuu wa Serikali na Msajili vyama vya siasa nao ni miongoni mwa waliopewa haki ya kuweka pingamizi dhidi ya mgombea yoyote.

"Uzoefu unaonesha kuwepo kwa malalamiko yanayotolewa katika kipindi cha uteuzi bila kuwasilishwa kwenye mamlaka sahihi za kisheria na bila kufuata hatua stahiki ikiwemo hii ya kuweka pingamizi.Katika hatua hii muweke pingamizi na aliyekuwekea pingamizi wanahaki ya kukata rufaa kwenye mamlaka husika pale ambapo hawataridhika na maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi,amesema.

Wakati huo huo Jaji Mstaafu Kaijage amesema katika kipindi cha kampeni, vyama vyao vitapata fursa ya kuwanadi wagombea na kueleza sera na Ilani za Uchaguzi za vyama vyao.Katika eneo hilouzoefu unaonesha kuwa kipindi cha kampeni kunakuwa na joto kali la kisiasa linatokana na baadhi ya watu kukosa uvumilivu wa kisiasa hali inayoweze kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

" Napenda kutoa rai kwenu na wafuasi wenu na kuwasihi kufanya kampeni za kistaarabu na hivyo kuepuka kufanya vitendo vitakavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi yetu,"amesema.


 CHANZO- MICHUZI BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527