CHADEMA KUKUTANA KWA SIKU TATU KUCHAGUA MGOMBEA URAIS, WABUNGE, MADIWANI


CHADEMA kinaingia siku tatu ngumu za mchakato wa kupata mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

 Chadema kitaanza mikutano yake kesho Jumapili tarehe 2-4 Agosti, 2020 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Pia, Chadema kitatumia mikutano hiyo, kuwapata wagombea ubunge, wawakilishi na madiwani wa viti maalum na wabunge wa viti maalum.
    
Kesho Jumapili, itakuwa ni kikao cha Kamati Kuu ya Chadema, Agosti 3, zamu ya Baraza Kuu na mwisho Agosti 4 itakuwa ni mkutano mkuu.

Awali, mikutano hiyo ilipangwa kufanyika kati ya tarehe 27 hadi 29 Julai 2020, lakini ikasogezwa mbele kutokana na msiba wa Hayati Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527