JAMBO YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA WANAWAKE 'SHINYANGA SUPER QUEENS'

Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd imetoa msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo jezi za kisasa kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Shinyanga Super Queens ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kushiriki michuano ya Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kwa soka la wanawake.

Shinyanga Super Queens ni timu pekee ya soka ya wanawake mkoani Shinyanga ambayo inajiandaa na Ligi daraja la kwanza ili kusaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (SWPL) msimu ujao.

Hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaa vya michezo imefanyika Agosti 10, 2020 katika ofisi kuu za kiwanda cha Jambo zilizopo Ibadakuli mjini Shinyanga.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Bi. Halima Omary Rashid alisema Kampuni ya Jambo imeona ni vyema kusaidia vifaa vya michezo ili kuongeza nguvu na kuwapa hamasa wachezaji wafanye vizuri katika michuano ya Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kwa soka la wanawake.

"Msaada huu hautoshi, tunapenda kuona wadau wengine wakijitokeza kuisaidia timu hii ambayo imeonyesha nia ya kung’arisha nyota ya mkoa wa Shinyanga katika medani za mpira wa soka la wanawake," alisema Halima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shinyanga Super Queens, Flora Gaguti aliishukuru Kampuni ya Jambo Food Products Ltd kwa kuishika mkono timu hiyo na kueleza kuwa timu iko vizuri na imara kushiriki vyema Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kwa soka la wanawake na matarajio yake ni kuupaisha mkoa wa Shinyanga katika medani za soka la wanawake kwa ushindi na kupanda daraja kwenda ligi kuu. 

Naye, Mkuu wa Shinyanga Super Queens, Henry Moroto ametamba kuwa timu yake iko imara na hakuna timu itakayoizuia kuubeba ushindi wa ligi hiyo, huku wachezaji nao wakitamba kuchukua ubingwa wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza siku za karibuni.

Katika makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa Timu ya Shinyanga Super Queens, pia Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, ilikabidhi vifaa vya michezo kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya wanaume maarufu Shinyanga Talent. 
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Food Products Ltd, Halima Rashid (kushoto) akimkabidhi jezi Nahodha wa timu ya Shinyanga Super Queens, Tatu Abbas 
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Food Products Ltd, Halima Rashid (wa pili kulia) akiendelea kukabidhi jezi mmoja wa wachezaji wa Shinyanga Super Queens. Kushoto ni wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Food Products Idara ya Masoko ambao ni Ophebia Juvenary,Zena Zaed na Alodia Kelvine.

Mkurugenzi wa Shinyanga Super Queens, Flora Gaguti akiishukuru Kampuni ya Jambo Food Products Ltd kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Bi. Halima Omary Rashid baada ya kukabidhi vifaa vya michezo ikiwemo jezi za kisasa kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Shinyanga Super Queens
Kocha Mkuu wa Shinyanga Super Queens, Henry Moroto akizungumza baada ya kupokea vifaa vya michezo ikiwemo jezi za kisasa.
Nahodha wa Shinyanga Super Queens, Tatu Abbas akiishukuru Kampuni ya Jambo Food Products Ltd kwa kuwapatia msaada wa jezi.
Wachezaji, viongozi wa Shinyanga Super Queens na wawakilishi kutoka Kampuni ya Jambo Food Products Ltd wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo.

Picha ya kumbukumbu wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa Timu ya Shinyanga Super Queens na Shinyanga Talent.
Picha ya kumbukumbu wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa Timu ya Shinyanga Super Queens na Shinyanga Talent.
Wachezaji, viongozi wa Shinyanga Talent na wawakilishi kutoka Kampuni ya Jambo Food Products Ltd wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527