RAIS MAGUFULI APEWA TUZO YA KUPAMBANA NA CORONA


Rais Magufuli wakati akikabidhiwa Tuzo na Askofu wa Kanisa la TAG Dkt Barnabas Mtokambali.
***
Baraza kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), limemkabidhi Tuzo maalum Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake katika kuliongoza Taifa kumtegemea Mungu katika kipindi cha janga la Virusi vya Corona nchini.

Tuzo hiyo amekabidhiwa leo Agosti 14, 2020, na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt Barnabas Mtokambali, katika Mkutano Mkuu wa Baraza kuu la Kanisa la TAG, wakati akifungua mkutano huo, uliofanyika Jijini Dodoma.

Aidha Askofu Mtokambali amesema kuwa jambo lililofanywa na Rais Magufuli katika kipindi kile la kuruhusu shughuli za kimaendeleo ziendelee kama kawaida, lilikuwa la tofauti kwani ni katika kipindi hicho ambapo Mataifa mengine yaliweka nguvu ya kuzuia watu wasitoke majumbani.
 Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post