WIZARA YA ELIMU YAZIELEKEZA SHULE ZOTE NCHINI KUFUATA RATIBA ZA MASOMO 8 KAMA ZAMANI


Wizara ya Elimu imetolea ufafanuzi ongezeko la saa 2 za masomo kwa Wanafunzi baada ya Shule zote nchini kufunguliwa ili kufidia muda ambao umepotea kutokana na mlipuko wa CoronaVirus.


Wizara hiyo imesema tathmini waliyofanya imebaini jambo hilo ni gumu kutekelezeka kwasababu kuna Shule zenye vibali vya kuendesha masomo kwa mfumo wa 'double shift'. Pia suala la usafiri kwa wanafunzi waishio mbali nalo limeonekana kuwa ni changamoto

Kutokana na hilo, Wizara imezitaka Shule kutumia ratiba za vipindi 8 kama ilivyokuwa awali na Shule zitakazoona umuhimu wa kuongeza muda wa masomo zitatumia muda uliopangwa kwenye ratiba zao


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527