TCRA YAZIPIGA FAINI YA MAMILIONI KAMPUNI ZA SIMU NCHINI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu kwa makampuni ya simu yafuatayo: Airtel Tanzania Plc, MIC Tanzania Plc, Smile Communications Tanzania Ltd, Tanzania Telecommunications Cooperation, Viettel Tanzania Plc, Vodacom Tanzania Plc, na Zanzibar Telecoms Plc kwa kutakiwa kulipa faini mbalimbali kutokana na makosa ya kutoweka vigezo na masharti sahihi, kwenye vifurushi, na bidhaa au huduma watoazo.

Hatua hii imefikiwa na TCRA baada ya kubaini kuwa makampuni tajwa ya Simu wamekuwa walikiuka Kanuni Na. 4 & 7(3) za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Ulinzi kwa Mlaji), 2018 na Kanuni Na. 12(4) ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Ushuru/tozo), 2018 pamoja na kutozingatia maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na TCRA.

Baada ya kubainika kwa ukiukwaji wa Kanuni hizo na kwa mujibu wa Kifungu cha 48 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Sura ya 172 marejeo ya 2017 ya Sheria za Tanzania, makampuni hayo; Airtel Tanzania Plc, Zanzibar Telecoms Plc, Viettel Tanzania Plc, MIC Tanzania Plc walitakiwa kufika mbele ya TCRA tarehe 11 Juni 2020 ilhali Vodacom Tanzania Plc, Tanzania Telecommunications Cooperation na Smile Communications Tanzania Ltd walifika tarehe 12 Juni, 2020, ili kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria na kikanuni kwa ukiukaji huo wa Kanuni. Makampuni hayo yalifika mbele ya TCRA kama yalivyoamriwa.

Baada ya TCRA kuzingatia utetezi uliotolewa na makampuni yote tajwa hapo juu na kujiridhisha kuwa ni bayana yamekiuka Kanuni, na kwa mujibu wa Kifungu cha 48 (2)&(3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Sura ya 172 marejeo ya 2017 ya Sheria za Tanzania, TCRA imetoa adhabu kwa makampuni hayo kama ifuatavyo: -

A. Airtel Tanzania Plc
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 350,000,000/= (Milioni Mia Tatu na Hamsini), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

B. MIC Tanzania Plc
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 300,000,000/= (Milioni Mia Tatu), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;
  
C. Smile Communications Tanzania Ltd
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 15,000,000/= (Milioni Kumi na Tano), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

D. Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 30,000,000/= (Milioni Thelathini), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

E. Viettel Tanzania Plc
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 130,000,000/= (Milioni Mia Moja Thelathini), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

F. Vodacom Tanzania Plc
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 400,000,000/= (Milioni Mia Nne), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

G. Zanzibar Telecoms Plc (ZANTEL)
1) Kulipa ndani ya siku kumi na nne (14) faini ya Shilingi 25,000,000/= (Milioni Ishirini na Tano), tu.
2) Kutakiwa kurekebisha makosa yaliyobainika na kutoa taarifa kwa TCRA namna walivyo ya shughulikia kabla ya tarehe 30 Julai, 2020;

Iwapo Makampuni hayo yatashindwa kutekeleza maagizo haya, TCRA itachukua hatua zaidi za kiudhibiti na kisheria pasipo kutoa taarifa zaidi na kwa gharama zao wenyewe.

IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
2 Julai, 2020

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527