WATANZANIA WATAKIWA KUEPUKA HABARI ZA UZUSHI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 29, 2020

WATANZANIA WATAKIWA KUEPUKA HABARI ZA UZUSHI

  Malunde       Wednesday, July 29, 2020

Watanzania wametakiwa kulisemea mambo mazuri Taifa lao ili kuwa na kidiplomasia nzuri na Mataifa mengine hususani wakati huu ambapo Taifa linaomboleza kifo Hayati Benjamini William Mkapa na kuachana na habari za upotoshaji zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii hasa baada ya ujumbe wa Kenya uliokuwa ushiriki katika maziko ya kitaifa Jijini Dar es Salaam kushindwa kufika kama ilivyokuwa imepangwa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Damas Ndumbaro ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kufuatia kuenea taarifa za uzuishi katika mitandao ya kijamii hususani baada ya ujumbe uliokuwa uiwakilishe Kenya katika maziko ya kitaifa yaliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kushindwa kufika na ndege iliyokuwa imewabeba wajumbe hao kurejea Kenya.

Dr.Ndumbaro ameongeza kuwa kuandika au kuchapisha taarifa za uzushi na zisizo na uthibitisho ni kinyume cha sheria za mitandao yam waka 2015 na adhabu yake ni pamoja na kifungo gerezani.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post