Picha : WANAFUNZI WALIOSOMA UHURU SEKONDARI WAMWAGA MISAADA KURUDISHA MAKALI YA SHULE YAO


Kiongozi Mkuu wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Uhuru mwaka 2004, Masasi Marco akimkabidhi Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi shuleni hapo, Ruth Joseph sehemu ya msaada kuboresha shule hiyo
Kiongozi Mkuu wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Uhuru mwaka 2004, Masasi Marco akimkabidhi Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi shuleni hapo, Ruth Joseph sehemu ya msaada kuboresha shule hiyo, wengine katika picha hiyo ni walimu wa shule hiyo.

Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club Blog
ILI kuhakikisha Shule ya Sekondari Uhuru iliyopo Manispaa ya Shinyanga mkoani humo inarejea katika makali yake kitaaluma, nidhamu na heshima iliyojengwa siku za nyuma, baadhi ya wadau mbalimbali waliowahi kusoma shuleni hapo wametoa msaada wa vifaa mbalimbali kukarabati baadhi ya majengo na fedha taslimu.

Umoja wa wanafunzi hao waliowahi kusoma shuleni hapo wamekabidhi fedha Sh 750,000/=, ndoo 18 za rangi kwa uongozi wa shule hiyo leo Julai 3, 2020 shuleni hapo, huku wakikutana na walimu wao wa zamani na kubadilishana mawazo na kuwapa mawaidha wanafunzi wanaoendelea na masomo katika shule hiyo.

Akikabidhi msaada huo, Kiongozi Mkuu wa wanafunzi waliosoma Uhuru Sekondari mwaka 2004, Misasi Marco alisema sehemu kubwa ya malengo yao ni kukusanyana na kuisaidia shule hiyo kutokana na wataalam mbalimbali waliozalishwa shuleni hapo mpaka sasa, kwani takwimu zinaonyesha idadi inafika wanafunzi 7,000 waliowahi kupita katika shule hiyo.

Marco amesema binafsi yuko tayari kutoa Sh 200,000 kwa mwanafunzi yeyote wa kidato cha nne katika shule hiyo atakayepata wastani wa kwanza (divion one) ya mwanzo kwenye mtihani wa taifa wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu.

"Japokuwa tumechelewa lakini tumeona kuna haja ya kuhamasisha wenzetu na kuweka mikakati na walimu namna ya kushiriki kuiboresha shule yetu," amesema.

Mmoja wa wanafunzi waliosoma shuleni hapo mwaka 2004, Estomine Henry ambaye kwa sasa ni Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mko wa Shinyanga (SPC), amewataka wanafunzi kudumisha nidhamu, kuzingatia masomo, kuweka ushindani chanya kwenye masomo ili kuipaisha shule yao kwani miaka ya nyuma shule hiyo ilisifika kwa ufaulu mzuri, heshima na bidii katika masomo.

Mwakilishi wa wanafunzi waliomaliza Uhuru Sekondari mwaka 1998, Nurah Kamuntu amesema tayari wameshashiriki katika kuiboresha shule hiyo kwa kupaka rangi madarasa, maabara na kufanya maboresho kwenye vyoo.

"Tuliwaza sana tutaifanyia nini shule yetu, ndipo tukaja na huu mpango wa kupaka rangi baadhi ya madarasa hapa shuleni na maabara, lakini pia tumeboresha vyoo na baadhi ya madarsa, hii yote ni kurudisha shukrani kwa jamii.....Shukrani hii ndogo tuliyoileta kwenu ni mwendelezo, je wewe (mwanafunzi) utarudisha shukrani ipi kwa shule yako," amesema.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhuru, Victoria Nakiliaumi amesema wadau hao wanaboresha mazingira ya shule hiyo ili kuinua taaluma, ambapo amewataka wanafunzi wake kuhakikisha wanalikamilisha lengo hilo.

"Hawa wenzenu walikuwa na nidhamu sana na bidii katika masomo, lazima na nyinyi muendeleze na mpite katika mkondo huo," amesema.

Mmoja wa walimu wakongwe na maarufu shuleni hapo, Wilfred Masanja ambaye ni mtunzi wa wimbo wa shule hiyo, baada ya kukutana na wanafunzi wake wa zamani na kupewa fursa ya kuzungumza, amewataka wanafunzi kudumisha nidhamu, kujiunga na klabu mbalimbali zinazoanzishwa shuleni hapo mfano Klabu ya Mali Hai iliyokuwa ikitunza mazingira ili kuisaidia shule, pia akawataka wadau wengine kuendelea kuisaidia shule hiyo.

"Tuwe na makambi ya kujisomea kama ilivyokuwa utamaduni wa shule yetu, nawaomba sana msome kilichokuleta hapa ni kusoma mna walimu wazuri na wanafundisha kwa bidii, msaada ulioletwa tuutumie vizuri kazaneni na muda uliotolewa uwasaidie katika maisha yenu.

"Haya yanayozungumzwa ni ya kukufanya ujitambue na yachukueni kwa uchungu mkubwa ili iweze kuwasaidia katika safari yenu ya kimasomo," amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu ilipo shule hiyo, Nassoro Warioba aliuomba uongozi wa shule kuendeleza mahusiano mazuri na wadau, huku akiwaomba wanafunzi hao wa zamani kuona uwezekano wa kulikamilisha jengo la maabara ambalo limejengwa na Serikali na sasa linahitaji kumaliziwa.

Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Shule ya Sekondari Uhuru, Ruth Joseph amewashukuru wote wanaoendelea kuisaidia shule yao, huku akisistiza kuwa kwa niaba ya wanafunzi wake wamepokea yale yote yaliyoelekezwa kwao na yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha kwamba heshima ya shule hiyo inaendelea kudumishwa.
Kiongozi Mkuu wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Uhuru mwaka 2004, Masasi Marco akizungumza shuleni hapo
Mratibu wa SPC, Estomine Henry akizungumza na wanafunzi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhuru, Victoria Nakiliaumi
Mwalimu Masanja akizungumza
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu, Nassoro Warioba
Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Sekondari ya Uhuru, Ruth Joseph
Wanafunzi wakimshangilia mwalimu wa zamani wa shule hiyo, Wilfred Masanja
Katibu wa Serikali ya Wanafunzi Shule ya Sekondari Uhuru, Ruth Joseph akipokea msaada wa ndoo za rangi 
Mmoja wa waliosoma shule ya sekondari Uhuru mwaka 2004, Estomine Henry akitoa ujumbe kwa wanafunzi
Mkuu wa shule ya sekondari Uhuru, Victoria Nakiliaumi na wanafunzi wake wakipokea sehemu ya msaada huo
Mmoja wa wanafunzi waliosoma shuleni hapo mwaka 1998, Nurah Kamuntu akizungumza na wanafunzi.
Kiongozi Mkuu wa wanafunzi waliomaliza Uhuru Sekondari mwaka 2004, Misasi Marco akimkabidhi Sh 750,000 mkuu wa shule hiyo, Victoria Nakiliaumi
Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhuru, Victoria Nakiliaumi akionyesha fedha alizopokea kutoka kwa wadau kuboresha mazingira ya shule hiyo
Baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kuboresha mazingira ya shule ya Sekondari Uhuru
Wanafunzi wakifuatilia tukio la kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kuboresha shule yao
Mwalimu wa zamani wa shule hiyo, Wilfred Masanja alifika kujumuika na wanafunzi aliowafundisha
Mmoja wa wanafunzi waliohitimu shuleni hapo mwaka 1998, Nurah Kamuntu (kushoto) akiteta jambo aliyekuwa mwalimu wa shule hiyo
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu, Nassoro Warioba naye alipata fursa ya kutoa shukrani za serikali ya mtaa.
Walimu wa Shule ya Sekondari Uhuru wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliojitokeza kusaidia shule hiyo
Wanafunzi wa Uhuru Sekondari wakisikiliza ujumbe
Wanafunzi wakifuatilia kwa ukaribu tukio la kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali
Wanafunzi wa shule hiyo
Wanafunzi wakifuatilia kwa umakini mkubwa ujumbe unaotolewa kwao
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hapo miaka ya nyuma wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu waliowafundisha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post