Breaking News : RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA WAPYA... AGGREY MWANRI, KUPUMZIKA,ANDENGENYE ALAMBA KIGOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Julai 3,2020 amefanya uteuzi wa Wakuu wa mikoa wawili ambapo amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Bw. Aggrey Mwanri ambaye amestaafu huku akimteua Bw. Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye amestaafu.

Rais Magufuli pia ameteua wakuu wa wilaya 9
1. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa kuwa mkuu wa wilaya ya Kilombero kuchukua nafasi ya James Mugendi ambaye amestaafu.
2. Jamila Yusuph kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kuchukua nafasi ya Lilian Charles Matinga ambaye amestaafu.

3. Mhandisi Martine Ntemo kuwa mkuu wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kuchukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

4. Salum Kali kuwa mkuu wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza akichukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora.

5. Wilson Samwel Shimo kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita.

6. Kanali Mathias Kahabi kuwa Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kuchukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

7. Abbas Kayanda kuwa mkuu wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha kuchukua nafasi ya Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu.

8. Lazaro Jacob Twange kuwa mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara kuchukua nafasi ya Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.


9. Toba Alnason Nguvila kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga kuchukua nafasi ya Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam. Godwin Gondwe anachukua nafasi ya Felix Jackson ambaye amestaafu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527