MAKADA 30 WA CCM LEO JULAI 14 WAMEOMBA KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 14, 2020

MAKADA 30 WA CCM LEO JULAI 14 WAMEOMBA KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI

  Malunde       Tuesday, July 14, 2020

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akizungumza na Malunde 1 blog leo majira ya saa 10 jioni ambapo alisema Jumla ya wanachama 30 wa Chama cha Mapinduzi wamejitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini ambapo kati yao wanaume ni 24, wanawake ni 6.Amewataja wanawake waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kuwa ni Grace Anthony Lyon, Eunice Jackson Wiswa, Veronica Shittah Milambo, Hamisa Boniphace Magulu, Lydia Winga Pius na Mary Paul Izengo.

Katibu huyo wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini amewataja wanaume waliochukua fomu kuomba kugombea jimbo la Shinyanga Mjini kuwa ni Stephen Julius Masele (anayetetea kiti chake),ambapo wengine ni Dotto  Joshua, Hassan Athuman Fatiu, Musa Jonas Ngangala,Benjamini Dionise Chagula, Bandora Salum Milambo, Ramadhan Hamis Ramadhan, Austin Makwaia Makani, Stanley Otto Mayunga, John Samwel Mlyambate, Severine Luhende Kilulya, Kulwa Ezekiel Mathias, Francis Gilya Kasili, Paul Itwelambuli Nangi na  Gratian Cronery  Rwekaza.

Wengine ni Leonard Ibrahim Mapolu, Godfrey Peter Msemakweli, Wilbeth Makulo Masanja, John Festo Makune, Erasto Izengo Kwilasa, Yonah Michael Mapesa, Jonathan Manyama Ifunda, Gaspar Hanson Kileo na Joab Ajuna Kaijage.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post