AHMED SALUM ARUDISHA FOMU YA KUGOMBEA TENA UBUNGE JIMBO LA SOLWA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum (CCM) akionesha fomu ya kuwania ubunge wa jimbo la Solwa  masaa mawili baada ya kuichukua.

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog

Ahmed Salum ambaye anatetea kiti chake amechukua fomu ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Solwa leo Julai 14, 2020 saa 2 asubuhi na kuirejesha saa 4 asubuhi  katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Salum amesema anawashukuru viongozi wa chama hicho kwa kutengeneza mfumo mzuri wa kidemokrasia katika kupata wagombea ambao unatoa demokrasia ndani ya chama.

“Kikubwa tuchukue fomu tujaze tumtangulize Mungu, tusubiri mchakato ndani ya chama endapo jina langu likipendekezwa kama mgombea wa CCM ndipo nitazungumza zaidi,” amesema.
Ahmed Salum akisalimiana na baadhi ya wanawake waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania udiwani (Viti maalum) jimbo la Solwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527