MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU YALIPA USHURU SH. BILIONI 1.5 KUCHANGIA MAENDELEO MSALALA NA MJI WA KAHAMA


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corporation  kupitia migodi yake ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu imekabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 (1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020.

Akikabidhi hundi hizo kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha leo Jumatano Julai 15,2020,Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu amesema lengo la migodi hiyo ni kuona mamlaka husika zinaelekeza fedha hizo katika miradi inayolenga kuwaletea maendeleo wananchi wanaozunguka migodi.

Busunzu alifafanua kuwa mgodi wa Buzwagi umelipa shilingi 1,159,817,107.83/= kwa halmashauri ya Mji wa Kahama huku mgodi wa Bulyanhulu ukilipa shilingi 376,004,787.02/= kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala.

“Migodi ya Twiga Minerals chini ya Kampuni ya Barrick nchini Tanzania hulipa ushuru wa huduma kila baada ya miezi sita kwa halmashauri ili ambazo migodi yetu inaendesha shughuli zake kulingana na mapato ya kila mwaka ambapo malipo haya ni kutekeleza hitaji la kisheria na ni sehemu ya mikataba ya makubaliano kati ya migodi na halmashauri husika”,aliongeza Busunzu.

“Tunatoa ushuru ili kuboresha utoaji wa huduma katika jamii zinazozunguka migodi katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu,afya na upatikanaji wa maji safi na salama”,alisema.

Aidha alisema licha ya migodi hiyo kulipa kodi stahiki bado imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa maendeleo kupitia sera yake ya maendeleo ya jamii ni kuwa ikiwa ni kuunda fursa endelevu za kiuchumi na maendeleo kwa katika jamii na kuinua uchumi wa wilaya na kuboresha ustawi wa maisha ya wenyeji.

Akipokea hundi hizo, Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha aliipongeza kampuni ya Twiga Minerals kwa kutoa ushuru wa huduma ikiwa ni zao la kwanza chini ya Twiga iliyotokana na ubia kati ya serikali na Barrick huku akiziagiza halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia fedha hizo kwa utaratibu utakaoleta tija kwa wananchi.

“Sisi tunataka fedha zinaenda kwenye miradi ambayo itakuwa na tija kwa ajili ya maendeleo ya vijana, watu wenye ulemavu,wanawake. Mkono wa serikali bado upo pale pale kuhakikisha fedha hizi zinakwenda kutekeleza ile miradi tuliyoikusudia”,alisema Macha.

Alisema fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo katika jamii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika sekta ya elimu,afya,maji na miradi mingine itakayogusa wananchi moja kwa moja.

Naye Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama, Joachim Simbila aliipongeza Kampuni ya Twiga Minerals kwa kulipa ushuru huku akiziomba halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia vizuri fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi iliyokusudiwa.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha hundi ya shilingi 1,159,817,107.83/= zilizotolewa na Mgodi wa Buzwagi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama, Underson Msumba. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama, Underson Msumba hundi ya shilingi shilingi 1,159,817,107.83/= zilizotolewa na Mgodi wa Buzwagi kwa halmashauri ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020. 
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha hundi ya shilingi shilingi 376,004,787.02/= zilizotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu kwa halmashauri ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 (1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020 zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corporation.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 (1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020 zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corporation.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 (1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020 zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corporation.
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama, Joachim Simbila akiipongeza Kampuni ya Twiga Minerals kwa kulipa ushuru na kuziomba halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia vizuri fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi iliyokusudiwa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corporation kupitia migodi yake ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu ikikabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 (1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiziagiza halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia fedha hizo kwa utaratibu utakaoleta tija kwa wananchi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527