TUNDU LISSU ATANGAZA RASMI KUREJEA NCHINI MWISHONI MWA MWEZI HUU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 4, 2020

TUNDU LISSU ATANGAZA RASMI KUREJEA NCHINI MWISHONI MWA MWEZI HUU

  Malunde       Saturday, July 4, 2020

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu amesema mwishoni mwa mwezi Julai, 2020 atarejea nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kisiasa. Amesema, atafanya hivyo ili aweze kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 28 na 29 Julai 2020.

Mikutano hiyo, pamoja na mambo mengine, itampitisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Mchakato wa uchakuaji na urejeshaji fomu za kuwania Urais wa Tanzania unaanza leo Jumamosi tarehe 4 hadi 19,2020.

Wagombea au mawakala wao watakuwa na fursa ya kuchukua fomu kisha kutafuta wadhamini 100 katika kila kanda kumi za chama hicho.

Lissu ni miongoni mwa wanachama ambao wamekwisha tia nia hadharani ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post