CHAMA CHA UDP CHATANGAZA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU

Chama cha United Democratic Party (UDP) kimetangaza rasmi kumuunga mkono mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020  endapo Chama chake cha CCM  kitampitisha kuwa mgombea.

Maamuzi hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo Jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wake katika kipindi cha miaka mitano.

"Namsifu Magufuli kuweka Mazingira mazuri hospitali karibu na wananchi,kutuimarishia miundombinu ya Barabara na Reli," amesema  John Cheyo na kuongeza kuwa

"Tumeamua kumuunga mkono Rais Magufuli endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post