MAKADA 60 WA CCM WACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI.....SOLWA 54 , KISHAPU 78 | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 17, 2020

MAKADA 60 WA CCM WACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI.....SOLWA 54 , KISHAPU 78

  Malunde       Friday, July 17, 2020

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya wanachama 60 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini katika zoezi la uchukuaji fomu lililoanza Julai 14,2020 na kuhitimishwa leo Julai 17,2020 majira ya saa 10 jioni.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga amesema kati ya wanachama 60 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu, wote wamerudisha wakiwemo wanawake ni  saba na wanaume 53.

Bwanga amesema Mkutano wa kura za maoni kuwapigia kura wagombea utafanyika Julai 20,2020.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Emmanuel Lukanda amesema jumla ya wanachama 54 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Solwa ambapo kati yao wanawake ni wanne na wanaume ni 50.

Kwa upande wa Jimbo la Kishapu jumla ya wanachama 78 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurudisha fomu za kuomba ridhaa CCM kugombea nafasi ya Ubunge ambapo kati yao wanawake ni wanne na wanaume ni 74.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post