HOTELI MPYA YA KISASA 'SHY PARK HOTEL' KUFUNGULIWA RASMI AGOSTI,2020 SHINYANGA MJINI...NAFASI ZA KAZI ZATANGAZWA

Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu ‘SHY PARK HOTEL’ ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 2020;  Mkurugenzi wa SHY PARK HOTEL anawatangazia nafasi za kazi wale wote waliosomea na wenye uzoefu wa Masuala ya Usimamizi wa Hoteli.

SHY PARK HOTEL IKO WAPI?
SHY PARK HOTEL inapatikana Lubaga Mjini Shinyanga karibu na Ikulu pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga.

HUDUMA ZINAZOPATIKANA SHY PARK HOTEL
Shy Park Hotel inatoa huduma za malazi ,vyakula, vinywaji, kumbi za sherehe/harusi na mikutano, Swimming pool kwa watoto na watu wazima, michezo mbalimbali ya watoto, Sauna, Massage, Gym, Car wash, Car Parking n.k

NAFASI ZA KAZI
Shy Park Hotel inakaribisha maombi ya kazi kwa waliosomea masuala ya Usimamizi wa Hoteli ‘Hotel Management na wenye uzoefu wa kutoa huduma tajwa hapo juu.

SIFA ZA WAOMBAJI WA KAZI
Sifa za muombaji awe na umri wa miaka kuanzia 20, awe na taaluma ya Usimamizi wa Hoteli ‘Hotel Management’ au mwenye uzoefu wa usimamizi wa hoteli. Watume maombi wakiambatanisha na barua ya udhamini iliyopitishwa na serikali ya mtaa.

KUTUMA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe ofisini, Fika SHY PARK HOTEL
Au kupitia  Email info@shypark.co.tz  au Whatsapp namba 0759096494
Kwa Mawasiliano zaidi piga simu namba 0621288344 

Mwisho wa kutuma maombi ni Julai 17,2020 saa sita mchana, usaili ‘Interview’ itafanyika Julai 18,2020

Karibu SHY PARK HOTEL
Picha mbalimbali muonekano wa majengo ya Shy Park Hotel iliyopo Mjini Shinyanga.


Muonekano wa vitanda
Muonekano sehemu ya Sauna

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post