RAIS MAGUFULI: SIJAMTUMA MTU KUGOMBEA UBUNGE NA HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ALIYEMTUMA MTU YEYOTE


Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amesema kuwa hadi Julai 16, 2020 asubuhi zaidi ya wanachama 8,000 wa chama hicho walikuwa wametia nia ya kugombea ubunge.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni ambapo ameeleza Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo unaongoza.

Aidha, Rais Magufuli ametumia wasaa huo kusisitiza kuwa taarifa kwamba baadhi ya watia nia wametumwa na viongozi wa serikali na chama akiwemo yeye na viongozi wengine wakiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM au Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wa vyombo vya ulinzi si za kweli.

Ametaka chama hicho kuwapima watia nia wote kwa usawa na kwamba wao hawajamtuma mtu, bali wanataka wananchi wachague wenyewe wa kumtuma.

Hata hivyo amesema uwepo wa idadi hiyo kubwa ya watia nia ni ishara ya kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama hicho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527