NHIF TANGA YAOKOA MILIONI 76, YATOA ONYO KWA VITUO


 Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Ally Mwakababu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kulia ni Mkuu wa Idara wa Bima katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Melinas Kidogoma

 Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Mkuu wa Idara ya Bima Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Melinas Kidogoma

 Mkuu wa Idara ya Bima Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Melinas Kidogoma akizungumza kulia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu

Mgonjwa ambaye ni mwanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akipimwa 
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kuokoa kiasi cha milioni 76 kutoka vituo vya kutolea huduma ambavyo vilionekana kuwa na mapungufu wakati wa kaguzi ambayo ililenga kuviongezea uwezo wa uelewa ikiwemo kuona taratibu wa matibabu zinafuatwa kama zilivyo za wizara 

Hatua hiyo ni kutokana na kufanya kaguzi 125 kwenye vituo vya kutoa huduma ambavyo bado vilionekana kuwa na mapungufu huku wakitoa onyo kwao iwapo wataendelea na vitendo vya namna hiyo watachukuliwa hatua kali. 

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Ally Mwakababu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alisema kaguzi hizo walizifanya ikiwa ni kuona kama vituo hivyo zinafuatwa taratibu za wizara. 

Alisema kwamba kufuatia uwepo wa mapungufu hayo mfuko huo umetoa onyo kali na iwapo vituo hivyo vitarudia makosa hayo watavipeleka vyombo vya sheria au kuvifungia. 

“Lakini niwaambie kwamba nia yetu sio kuvikomoa vituo ila kuhakikisha huduma za msingi stahili stahiki zinatolewa kwa wananchi kwa sababu nhif imetoa ahadi kwa kwao ukiwa ndani ya mfuko unapata kila kitu hivyo anapokosa kwa sababu yako Lazima uwajibishwe”Alisema Meneja Mwakababu. 

Awali akizungumza katika mkutano huo, Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza alisema kwamba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inakaribia kusajili duka dawa la ndani na ipo kwenye hatua za mwisho na hiyo itapunguza usumbufu kwa wanachama ambao lazima walikuwa watoke nje ya geti kuchukua vifaa na kurudi ndani kupata huduma.



Alisema kwamba hospitali wameanzisha mradi huo wanatarajia kuwa duka hilo litasaidia kuondoa usumbufu ambao walikuwa wakikumbana nao wanachama wao. 

Hata hivyo alisema suala la udanganyifu kwenye uwasilishwaji wa madai fedha zinazolipwa kwa kufauta miongozo na taraibu ambazo zimewekwa huku akieleza kwamba watoa huduma wa namna hiyo hawawezi kuwavumiliwa na watachukuliwa hatua. 

“Kwa kweli tunapobaini madai yana udanganifu hatuchelewi kuchukua hatua kwa watoa huduma na wanajua tunavamia vituo tujiridhishe anachodaia ni kweli”Alisema 

Daktari huyo alisema kwani wakiwapa nafasi watoa huduma ambao sio waaminifu wanachukua nafasi ya kujiongezea vitu ambyao wanachama wao hawajapata kwenye vituo vyao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527