MWILI WA RAIS MSTAAFU, BENJAMIN MKAPA KUWASILI MOJA KWA MOJA KIJIJINI LUPASO BADALA YA NACHINGWEA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 27, 2020

MWILI WA RAIS MSTAAFU, BENJAMIN MKAPA KUWASILI MOJA KWA MOJA KIJIJINI LUPASO BADALA YA NACHINGWEA

  Malunde       Monday, July 27, 2020

Mwili wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa utawasili moja kwa moja kijijini Lupaso, mkoani Mtwara kesho jioni kutoka jijini Dar es Salaam tayari kwa maziko yatakayofanyika Julai 29.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa wakati akieleza kuhusu maandalizi ya maziko ambayo amesema hadi sasa yamefikia asilimia 80.

Byakanwa amesema kuwa ratiba imebadilika ambapo awali mwili ulikuwa ushushwe Uwanja wa Ndege wa Nachingwea mkoani Lindi na kisha upelekwa kijijini kwao, lakini sasa utatolewa Dar es Salaam hadi Lupaso.

Amesema taratibu za kuhakikisha kunapatikana malazi na usafiri kwa wageni wote watakaofika bado zinaendelea.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post