MWANASHERIA AKARO-SIMBA RICHMOND ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA


Mwanasheria Akaro-Simba Richmond  amechukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 

Simba amekabidhiwa fomu hiyo leo Ijumaa tarehe 10 Julai 2020 katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam na  Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema  Reginald Munisi

 
Mtia nia huyo anakuwa wa saba ndani ya Chadema kugombea Urais wa Tanzania, tangu zoezi hilo lianze tarehe 4 Julai 2020. Zoezi hilo litafungwa tarehe 19 Julai mwaka huu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527