MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) DKT HUSSEIN MWINYI ASISITIZA USHIRIKIANO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 10, 2020

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) DKT HUSSEIN MWINYI ASISITIZA USHIRIKIANO

  Malunde       Friday, July 10, 2020

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Hussein Mwinyi amesisitiza ushirikiano na mshikamano ndani ya chama hicho wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.

Amesema ushirikiano na mshikamano ndio utakaokiwezesha chama hicho kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kwa pande zote mbili za muungano.

Dkt Mwinyi ameyasema hayo jijini Dodoma mara baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata kura 129 kati ya kura zote zilizopigwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa jijjni Dodoma.

Dkt Mwinyi amewashinda Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16 na Dkt Khalid Salim Mohamed aliyepata kura 19.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post