MAANDALIZI YA MAZISHI YA RAIS MKAPA YAKAMILIKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 27, 2020

MAANDALIZI YA MAZISHI YA RAIS MKAPA YAKAMILIKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50

  Malunde       Monday, July 27, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema kuwa maandalizi ya mazishi ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 50.

Akizungumza na TBC katika Ikulu ndogo ya Mtwara, Byakanwa ameeleza kuwa wameandaa utaratibu wa usafiri wa kutoka Masasi kwenda kijijini Lupaso kwenye mazishi ili kuepusha kila mtu kutumia gari lake kufika huko.

Hata hivyo amesema kuwa utaratibu huo hautazuia watu kwenda na magari yao, lakini lengo lao ni kupunguza idadi ya magari yanayokwenda huko ili kuruhusu watu wengi zaidi kukusanyika.

Aidha, amesema serikali ya mkoa imeandaa utaratibu wa maeneo ya malazi kwa watu watakaokuja katika mazishi ya Rais Mstaafu, na amewahakikishia wote usalama wa kutosha katika kipindi chote watakachokuwa mkoani hapa.
Credit: TBC


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post