DC KATAMBI AJITOSA UBUNGE SHINYANGA MJINI.....HAYA HAPA MAJINA 48 MAKADA WA CCM HADI LEO WANAOUTAKA UBUNGE SHINYANGA MJININa Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi leo Jumatano Julai 15,2020 amechukua Fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya idadi ya wanachama wa CCM waliochukua fomu kufikia 48 hadi leo majira ya saa 10 jioni.Mwaka 2015 akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi aligombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA,hata hivyo Stephen Masele (CCM) aliibuka mshindi kiti cha Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na mwaka 2017 Katambi alijiunga CCM na baadaye kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma.

Leo wanachama 18 wa CCM wamechukua fomu kuomba kugombea ubunge kupitia CCM ambapo jana Julai 14,2020 waliochukua walikuwa 30 hivyo kufanya idadi kuwa 48.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu amesema jumla ya wanachama 18  wa CCM wamejitokeza kuchukua fomu   kuomba kugombea ubunge kupitia CCM leo Julai 15,2020 ambao ni Joseph Ernest Kimaro, Isaack Elias Tungu,Robert David Budulabu, Meshack Elias Mashigala,Kashi Salula Gacha, Shiwa Maduhu Jasamila,Emmanuel Anthony Mwikabe,Makoye Richard Kashinje, Valerian Senduye Baleke, Yusuph John Mbundi, Abdulmalik Ibrahim Hassan,Frank Peter Alex, Mpanga Paulo Mpanga, Patrobas Paschal Katambi,Jitomoli Julala Maduka,Elzeus Alphonce Rwehumbiza, William Festo Makune na Emmanuel Alex Kiberiti 

Waliojitokeza kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Julai 14,2020 ni 30 kati yao wanawake ni 6 ambao ni  Grace Anthony Lyon, Eunice Jackson Wiswa, Veronica Shittah Milambo, Hamisa Boniphace Magulu, Lydia Winga Pius na Mary Paul Izengo.


Wanaume waliochukua fomu ni Stephen Julius Masele (anayetetea kiti chake),ambapo wengine ni Dotto Joshua, Hassan Athuman Fatiu, Musa Jonas Ngangala,Benjamini Dionise Chagula, Bandora Salum Milambo, Ramadhan Hamis Ramadhan, Austin Makwaia Makani, Stanley Otto Mayunga, John Samwel Mlyambate, Severine Luhende Kilulya, Kulwa Ezekiel Mathias, Francis Gilya Kasili, Paul Itwelambuli Nangi na Gratian Cronery Rwekaza.

Wengine ni Leonard Ibrahim Mapolu, Godfrey Peter Msemakweli, Wilbeth Makulo Masanja, John Festo Makune, Erasto Izengo Kwilasa, Yonah Michael Mapesa, Jonathan Manyama Ifunda, Gaspar Hanson Kileo na Joab Ajuna Kaijage.


Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akimkabidhi Patrobas Katambi fomu ya kuomba ridhaa kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Picha na Marco Maduhu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527