CHARLES MWIJAGE AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI JIMBO LA MULEBA KASKAZINI

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda nchini na Mbunge wa Muleba Kaskazini mkoani Kagera mh Charles Mwijage (CCM) ameibuka kidedea katika kura za maoni jimboni humo.

Mwijage amepata kura 387 na kuwashinda wapinzani wake 19 alioingia nao katika kinyang'anyiro hicho cha kumtafuta mshindi katika kura za maoni kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

Katika kinyang'anyiro hicho wa pili ni bwana Edward Mujungi amepata kura 135 na Adonisia Bitegeko amepata kura 30.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post