ALICHOKISEMA MAKONDA BAADA YA KUSHINDWA KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA KIGAMBONI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 21, 2020

ALICHOKISEMA MAKONDA BAADA YA KUSHINDWA KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA KIGAMBONI

  Malunde       Tuesday, July 21, 2020

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amewashukuru wale wote waliompa pole baada ya matokeo ya jana aliyoyapata kwenye kura za maoni Jimbo la Kigamboni na kusema kuwa jambo moja muhimu ni kuyajua mapenzi ya Mungu. 


Katika Matokeo hayo, Makonda alipata kura 122 huku Dk. Ndugulile akiongoza kwa  kura 190

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda ameandika: “Nimepata pole nyingi sana kutokana na Matokeo ya jana, kwanza nawashukuru kwa upendo wenu na maombi yenu ya kunitakia mafanikio katika kutimiza NDOTO yangu

“Jambo moja kubwa na muhimu ni kuyajua mapenzi ya Mungu na katika hili Mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu, nawatakia baraka na afya njema siku zote za maisha yenu

“Asanteni sana sana wanakigamboni kwa upendo wenu na kunipa nafasi niwe sehemu ya Maisha yenu” – Paul Makonda


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post