WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU ASHINDA KWA KISHINDO KURA ZA MAONI TANGA MJINI



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa kura za maoni Jimbo la Tanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 783 kati ya 880. Omary Ayoub amekuwa wa pili kwa kura 41 na wa tatu ni Juma Kimwaga amepata kura 33.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Kura za maoni Jimbo la Tanga Mjini alikuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella.

Picha na Oscar Assenga - Malunde 1 blog Tanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527