KADA WA CCM ABEL JOEL KAHOLWE ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINIKada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 17,2020. 


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Abel Joel Kaholwe ambaye ni Afisa Mtendaji kata ya Ntobo halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga amechukua na kurudisha fomu leo Ijumaa Julai 17,2020 asubuhi katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Kaholwe ambaye aligombea udiwani kata ya Ndala katika jimbo la Shinyanga mwaka 2015 amesema mwaka huu amejitolea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika nafasi ya Ubunge ili kuendelea kusukuma gurudumu mbele la maendeleo. 

“Mimi ni kada mkongwe wa CCM ambaye chama kimekuwa kikiniamini tangu mwaka 2015 ambapo katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kilinipa dhamana ya kupeperusha bendera ya CCM kata ya Ndala. Kwa sasa wote tumeshuhudia kwa miaka hii mitano ya Rais John Pombe Magufuli amekuwa akifanya kazi kubwa sana na ameendelea kuwaamini vijana”,amesema Kaholwe.

“Mimi kama kijana nimejitolea kuja kuwatumikia wananchi wenzangu wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika nafasi ya Ubunge nikiamini kuwa yapo mambo mengi yameshafanywa na walionitangulia lakini zipo kasoro ndogo ndogo za kurekebisha kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo. Shinyanga ni Potential na inahitaji vijana Potential wenye uzalendo wa kuwatumikia wana Shinyanga”,ameongeza Kaholwe.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akionesha  fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini baada ya kuchukua katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, leo Julai 17,2020.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 17,2020. 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 17,2020. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post