Angalia Picha : RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUUAGA MWILI WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPARAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Kitaifa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam . PICHA NA IKULU
MAKAMU wa Rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan , akitowa heshima ya mwisho kwa mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Kitaifa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam 
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa hashima ya mwisho kwa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa marehemu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo 28/7/2020.(Picha na Ikulu)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifuta machozi wakati akielezea namna alivyomjua Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati akihutubia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, iliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
BAADHI ya Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao Nchini Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam 
MJANE wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akitowa heshima yake ya mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa hafla ya Kitaiga ya kuuaga mwili huo iliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

BAADHI ya Wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali Nchini Tanzania wakishiriki katika hafla ya kuuaga Mwili wa Hayati Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Willian Mkapa, iliofanyika Kitaifa leo  katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
MSAFARA wa gari maalum   ya JWTZ ikiwa imeubeba Mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapoa ukiwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutowa heshema ya mwishi kwa Viongozi wa Kitaifa na Wageni waalikwa.
MKE wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Benjamin Willian Mkapa, Mama Anna Mkapa (aliyejivunikakitambaa cheusi)  akiwa na Wanafamilia baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kutowa heshima za mwisho kwa Viongozi Wakuu na wageni kutoka nja ya Tanzania
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi katika jukwaa kuu wakati ukiwasili msafara uliochukua mwili wa Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla kuuanga kwa Viongozi wa Kitaifa (kushoto kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na (kulia kwa Rais) Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe.  Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, wakiwa wamesimama wakati wa kuwasili kwa msafara huo
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (kulia kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Rais Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Nne Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, wakiwa kjatika jukwaa kuu wakati ukipigwa wimbo wa Taifa, katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa Marehemu Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo 
WAGENI Waalikwa na Wananchi na Viongozi wa Serikali na JWTZ wakitowa salute wakati ukipigwa wimbo wa Taifa katika Uwanja wa Taifa Jijini Da es Salaam baada ya kuwasili kwa mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Benjamin William Mkapa, wakati wa hafla ya Kitaifa kwa Viongozi Wakuu kuuaga mwili wa mnarehemu 
BAADHI ya Mawaziri wa SMZ na SMT na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa  katika hafla ya kuuanga Mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Benjamin William Mkapa
VIONGOZI wa Jukwaa Kuu wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muunganio wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia kwa Waziri Mkuu) Waziri Mkuu wa Burundi. Jenerali Alain Guillaume Bunyoni , Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania  Bara. Mhe. Philip Mangula na Waziri Mkuu Mstaaf Edward Lowasa
BAADHI ya Viongozi wa Serikali na Mawaziri wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli(hayupo pichani ) akihutubia katika hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, iliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam 
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Rais Mstaaf wa Tanzania wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin Mkapa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwahutubia Wananchi katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo 28/7/2020, katika hafla ya Kitaifa ya kuuanga mwili wa marehemu
WAZIRI Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni, akizungumza na kutowa salamu za Nchi yake wakati wa hafla hiyo ya Kitaifa ya kuuanga mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Benjamin Willian Mkapa, iliofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
KIONGOZI wa Mabalozi Nchini Tanzania Balozi wa Comoro Nchini Tanzania akitowa salamu wakati wa hafla ya kuuaga mnwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu Tanzania. Benjamin William Mkapa, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post