WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS' WAKUTANA DODOMA .....WAKILI JAMES MARENGA ASISITIZA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Wakili wa Kujitegemea James Marenga wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unaotekelezwa na Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel jijini Dodoma.
*****

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wametakiwa kuwa mstari wa mbele zaidi kuzingatia maadili ya uandishi wa habari ikiwamo kuandika habari za ukweli na uhakika ili kuepusha upotoshaji na kujiingiza katika migogoro.Rai hiyo imetolewa leo Jumatatu Julai 27,2020 na Wakili wa Kujitegemea James Marenga wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unaotekelezwa na Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika ukumbi wa Royal Village Hotel jijini Dodoma.

Marenga alisema kati ya waandishi wa habari wanaotakiwa kuandika habari kwa usawa na ukweli zaidi ni waandishi wa habari wa mtandaoni kwa sababu wao wamekuwa wakiripoti matukio papo hapo mara tu matukio yanapotokea.

“Kama unaandika habari mtandaoni suala la maadili ya uandishi wa habari ni muhimu sana na haliepukiki. Waandishi wa habari Mtandaoni ambao wanajulikana kama ni Waandishi wa habari za Chap Chap mtandaoni wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maadili ya uandishi wa habari ikiwemo kuandika habari za ukweli na uhakika ili kuepuka kujiingiza katika matatizo”,alisema Marenga.

Pia, Marenga aliwataka waandishi wa habari kutochanganya uandishi wa habari na siasa huku akisisitiza kuwa endapo mwandishi wa habari anataka kujihusisha na masuala ya siasa basi aachane na uandishi wa habari.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club - APC) ambayo ni msimamizi wa mradi, Claud Gwandu aliwataka Waandishi wa Habari kufuata sheria zilizipo hata kama hawakubaliani nazo wakati asasi zao zikiwasiliana na Serikali kuangalia namna bora ya kurekebisha sheria hizo.

Awali, Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim aliwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania.

Afisa Mipango wa Arusha Press Club, Seif Mangwangi alisema miongoni mwa malengo ya kikao hicho cha Midterm Review ni kupitia mafanikio, changamoto na matarajio ya baadae ya mradi tangu ulipoanza Machi 2019, wanakundi kutunga kanuni na mwongozo zitakazosimamia kundi hilo la waandishi wa habari mtandaoni ili kutoa matokeo yanayotarajiwa na kupitia mwongozo wa wanahabari watakaokuwa wakiutumia kwenye shughuli zao za kila siku za kihabari ambao umetengenezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi. 

Alisema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT na unasimamiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (APC).
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Wakili wa Kujitegemea James Marenga wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unaotekelezwa na Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel jijini Dodoma.
Picha zote na Kadama Malunde & George Binagi - Malunde 1 blog
Wakili wa Kujitegemea James Marenga akiwasisitiza Waandishi wa Habari Mtandaoni kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club - APC) ambayo ni msimamizi wa mradi, Claud Gwandu akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) ambapo aliwataka Waandishi wa Habari kufuata sheria zilizipo hata kama hawakubaliani nazo wakati asasi zao zikiwasiliana na Serikali kuangalia namna bora ya kurekebiha sheria hizo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club - APC) ambayo ni msimamizi wa mradi, Claud Gwandu akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).

Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).

Afisa Mipango wa Arusha Press Club, Seif Mangwangi akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).
Afisa  Programu wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media)  kutoka taasisi za Freedom House, Lina Muro akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA).

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wakiwa katika picha ya pamoja.

Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wakiwa katika picha ya pamoja.
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha zote na Kadama Malunde & George Binagi - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post