Picha : YANGA YAJINOA FRESHO COMPLEX KUKIPIGA NA MWADUI FC CCM KAMBARAGE


Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Kikosi cha Yanga kikijifua kwenye uwanja wa Fresho Complex mjini Shinyanga

Na Damian Masyenene – Shinyanga Press Club Blog
Baaada ya kuwasili jana Juni 10, 2020 usiku mkoani Shinyanga, leo Alhamisi Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imefanya mazoezi kwenye uwanja mpya wa kisasa wa Fresho Complex nje kidogo ya mji wa Shinyanga kwa ajili ya kujiweka sawa kuwakabili wapinzani wao, Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) utakaopigwa Jumamosi Juni 13, 2020 kwenye dimba la CCM Kambarage.

Katika mazoezi hayo yaliyoanza saa 10 na kumalizika saa 12 jioni, Wana Jangwani hao waliongozwa na Kocha Msaidizi, Charles Boniphace Mkwasa pamoja na mwalimu wa magolikipa, Peter Manyika, huku wakiwakosa baadhi ya Wachezaji akiwemo Winga machachari, Bernad Morrison, nahodha Pappy Tshishimbi na beki Lamine Moro.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniphace Mkwasa alisema kuwa Kocha mkuu wa timu hiyo, Luc Eymael ataungana na kikosi chake kesho Ijumaa akiambatana na baadhi ya Wachezaji ambao hawajaungana na timu, huku akieleza kuwa nahodha Tshishimbi ataukosa mchezo huo kutokana na kadi tatu za njano alizonazo.

Pia Mkwasa ameeleza kuwa beki wao, Lamine Moro naye anasumbuliwa na majeraha hivyo hataungana na wenzake kwa ajili ya mchezo huo, huku kukiwa na habari njema za kuendelea vizuri kiafya kwa kiungo Abdulaziz Makame ambaye alijifua kivyake baada ya majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kirafiki mwishoni mwa wiki.

“Tunawaomba mashabiki wa timu yetu wajitokeze kwa wingi9 siku ya Jumamosi kuishuhudia timu yao na kuipa nguvu, kama tunavyofahamu nafasi hii ya mashabiki kuiona timu yao hapa Shinyanga ni adimu hivyo waitumie kuipa nguvu.

“Kikosi kinaendelea vizuri, Wachezaji wako salama na tulifika salama baada ya matatizo ya njiani yaliyotupata Singida na Shinyanga, kikubwa mwalimu wetu ataungana na timu kesho pamoja na Wachezaji wengine,” amesema Mkwasa.

Yanga ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wataendelea na mazoezi kesho Ijumaa kwenye dimba la CCM Kambarage kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mwadui.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kutazama timu ya Yanga ikifanya mazoezi wakiwa wamekwama nje ya geti la uwanja wa Fresho Complex baada ya kuzuiwa kuingia ndani.
Wachezaji wa Yanga wakipasha misuli
Mchezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (wa pili kutoka kulia) akijifua na wenzake kwenye uwanja wa Fresho Complex
Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi kwenye dimba la Fresho Complex mjini Shinyanga
wachezaji wakisikiliza maelekezo kutoka kwa walimu
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Ivory Coast, Yikpe Gramien akijifua na wenzake
Beki wa Yanga, Said Makapu ( wa pili kutoka kulia) akipasha misuli na wachezaji enzake akiwemo Balama Mapinduzi na Patrick Sibomana.
Wachezaji wa kikosi cha Yanga wakiendelea kujifua kwenye uwanja wa Fresho Complex mjini Shinyanga.
Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akiwania Mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Fresho Complex mjini Shinyanga
Mazoezi yakiendelea
Mlinda Mlango wa Yanga, Metacha Mnata akiwasili uwanjani hapo kwa usafiri wa pikipiki kuungana na wenzake kwenye mazoezi hayo.
CHANZO- SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527