TANGA UWASA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI KUENDELEZA HUDUMA YA MAJI MARUNGU



Mkuu wa Kitengo cha Ufundi Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shabani akizungumza wakati wa mkutano huo

Afisa huduma kwa Wateja Tanga Uwasa ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja Rogers Machaku akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto anayemfuatilia kwa umakini ni
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo
sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imesema kwamba watatumia fedha za ndani kuendeleza mradi wa maji Marungu kadri watakavyoweza ili mabomba yaweze kuwafikia wananchi kwa ukaribu ili wanapoomba kuunganishiwa huduma hiyo iwe karibu kuliko ilivyo sasa.

Mradi huo ulianza mwaka 2013 kwa ufadhili wa Serikali kupitia Programu endelevu katika sekta ya maji ukisimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga kabla ya Tanga Uwasa kukabidhiwa mwaka huu ili kuweza kuusimamia mradi huo na kuuendeleza

Hayo yalisemwa na Mhandisi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shabani katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na viongozi wa kata hiyo ambapo mamlaka hiyo ilipata nafasi ya kualikwa kuhudhuria na kuweza kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya maji.

Alisema baada ya kukabidhiwa mradi huo hivi sasa wanaangalia miundombinu iliyokuwepo na mahitaji yaliyopo katika mji wa Marungu ili kuanza mara moja shughuli za uendelezaji wa mradi huo ili kuweza kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi hatua itakayosaidia kuondosha kero hiyo.

“Mradi huu baada ya kukabidhiwa sasa tumejipanga kutumia fedha za ndani kadri tuwezavyo kuendeleza mradi huu na mabomba kuwafikia wananchi kuwaunganishia maji kwa karibu kuliko ilivyo sasa hivi inaonekana bombo limepita kwenye njia moja na ni kuu hivyo kwa mtu anayetaka maunganisho nyumbani kwaka anaweza kuwa mbali hivyo tutaendeleza yaweze kupita kwenye mita mbalimbali”Alisema

Hata hivyo Mhandisi huyo aliwataka wananchi wanaoomba maji kuhakikisha barua zao zinapita kwenye uongozi wa mtaa au kata ili kudhibitisha anapokaa ni kwake kwa sababu wanaweza kuomba ukakuta kiwanja kina mgogoro na wao hawataki kuweka miundombinu eneo lenye mgogoro kwa sababu hizo ni fedha za serikali na ukiwekeza sehemu ambayo sio sahihi utapata hasara.

Mhandisi huyo alisema tayari wataalamu wao wamekwisha kufika kwenye maeneo hayo kuweza kuona vioski vya kuchotea maji vinasimamiwa na watu gani na hayo maji wamepewa dhamana ya kuyasimamia na ikifika wakati wanaulizwa namna walivyousimamia na kufikisha huduma kwa wananchi.

Awali akizungumza katika mkutano huo Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea aliishukuru Tanga Uwasa kwa kufika kwenye mkutano huo baada ya kuwafuata ombi lake la kuwataka wataalamu wa mamlaka hiyo kuewaeleza wananchi ni lini wanaweza kufanikiwa kufikishia maji majumbani mwao.

“Nishukuru kwenye Kata yangu maji yamefika lakini hakuna mwananchi ambaye amwezea kuunganishiwa maji nyumbani kwake nah ii imekuwa ni kero kubwa hivyo tukaona tuwaalike kulizungumzia suala hilo ili liweza kupatiwa ufumbuzi “Alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527