RAIS MAGUFULI: TUTAFUNGUA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA CHEKEKEA HIVI KARIBUNI


Rais wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema atafungua shule za msingi na sekondari hivi karibuni, kama ataridhishwa na kasi ya upunguaji wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jijini Dodoma.

Amesema, maambukizi ya corona yamekuwa yakipungua siku hadi siku huku akiendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari  ya ugonjwa huo.

Huku akishangiliwa na umati wa mkutano huo,  Rais Magufuli amefurahishwa na washiriki wa mkutano huo walioujaza uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutokuvaa barakoa huku akionyesha kushangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuvaa barakoa akiwa ndani ya Bunge. 


“Corona imekwisha ndiyo maana hata mabarakoa hakuna, hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndiyo maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu."-Amesema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527