" Tanzia : ALIYEKUWA MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA WILE MZAVA AFARIKI DUNIA

Tanzia : ALIYEKUWA MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM SHINYANGA WILE MZAVA AFARIKI DUNIAAliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Wile Mzava ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Sereva Mjini Shinyanga, Wile Mzava amefariki dunia. 

Taarifa za awali zinasema Wile Mzava amefariki dunia ghafla leo Alhamis Juni 11,2020 majira ya saa tatu asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga.

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Nassoro Warioba chanzo cha kifo bado hakijajulikana na mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu amethibitisha taarifa za Kifo cha Wile Mzava.

Tutawaletea taarifa zaidi

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527