MTOTO AFARIKI DUNIA KWA KUSHAMBULIWA NA FISI KWIMBA

Mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Dalaile Milambo (6) mwanafunzi wa chekechea, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza amefariki baada ya kushambuliwa na fisi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP. Muliro Jumanne amesema tukio hilo lilitojea Juni 22, mwaka huu saa moja jioni katika Kijiji cha Mwampuru Kata ya Mwantare wilayani Kwimba.

Muliro amesema mwanafunzi huyo wa shule ya chekechea ya Mwampuru alifariki baada ya kushambuliwa na fisi sehemu mbalimbali za mwili wake wakati alipokuwa na dada yake.

Amesema, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Wanyamapori na wananchi wanamsaka fisi huyo ili adhibitiwe kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha kuwa haleti madhara zaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527