MSANII VITALI MAEMBE AJIUNGA ACT -WAZALENDO NA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 29, 2020

MSANII VITALI MAEMBE AJIUNGA ACT -WAZALENDO NA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE

  Malunde       Monday, June 29, 2020

Mwanamuziki  Vitalis Maembe amejiunga na Chama cha ACT-Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu.

 


Maembe  amejiunga na chama hicho leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 na kukabidhiwa kadi na Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa chama hicho, makao makuu ya ACT-Wazalendo, Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Maembe amesema ACT-Wazalendo ni chama chenye sifa anazozihitaji kama vile yeye anavyojipambanua kwenye muziki wake.


Akimkabidhi kadi ya uanachama Jana jijini Dar es Salaam , Ado amemuhakikishia Maembe kuwa ACT Wazalendo litakuwa jukwaa sahihi kwake kuendeleza mapambano ya kudai haki.

Amesema, zaidi ya haki ataendelea kupinga rushwa na kupigania umoja wa Afrika kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote kupitia sanaa.

Mbali na kuchukua kadi hiyo lakini pia Maembe aliyewahi kuimba nyimbo ya “Sumu ya teja”, “vuma” ametangaza nia ya kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Bagamoyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post