SPIKA NDUGAI APIGA MARUFUKU KUMJADILI KIGOGO WA TWITTER BUNGENI



Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewazuia Wabunge ndani ya Bunge hilo kutaja jina la Kigogo.

Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Juni 5, 2020, wakati Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, akichangia hoja ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo na ndipo alipotolea mfano wa baadhi ya watu kwamba wamekuwa wakikamatwa na kutakiwa kumtaja mtu anayetumia jina la Kigogo katika mtandao wa Twitter.

Mbunge Lema alisema kuwa "Waacheni watu mitandaoni wapumue, wanachosema kama siyo ukweli Waziri atoke ajibu, nyie mnasemwa sababu ni Serikali, na sisi tukiwa Serikali tutasemwa kwa kiwango chenu, mimi siyo Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa sasa waniseme kwa kipi, sasa Mheshimiwa Spika mkiwazuia nini kinatokea, siku hizi watu wengi wanakamatwa Kigogo ni nani Kigogo ni nani".

Mara baada ya Mh Lema kutoa kauli hiyo, Spika Ndugai akajibu, "Aaah nimepiga marufuku, huyo achana naye".

TAZAMA VIDEO HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527