
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Viongozi Watatu Mkoani Arusha na kufanya uteuzi wa viongozi watakaoshika nafasi hizo.
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kumteua Idd Kimanta kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Arusha mkoani Arusha, Gabriel Daqarro na nafasi yake kushikwa na Kenan Kihongosi. Hali Kadhalika ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni na kumteua Dkt. John Pima kushika nafasi hiyo.

Social Plugin