AGAPE YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTOA MSAADA KIFAA CHA KUNAWIA MIKONO SHULE YA MSINGI LUBAGA



Shirika lisilo la kiserikali la Agape linalotetea haki za watoto mkoani Shinyanga, limetoa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono katika shule ya msingi Lubaga iliyopo mjini Shinyanga, kwa ajili ya wanafunzi kunawa mikono ili kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Akizungumza leo Juni 16, 2020 wakati wa kukabidhi kifaa cha kunawia mikono, Mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola amesema wametoa kifaa hicho kama sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, ambapo pia Rais John Magufuli ameshatangaza kuwa shule zifunguliwe Juni 29 mwaka huu, ndipo wakaona ni vyema kuendelea kuwalinda wanafunzi dhidi ya Corona.

Amesema shirika hilo linalohusika na masuala ya utetezi wa haki za watoto limeguswa na kuanza kutoa vifaa vya kisasa mashuleni kwa ajili ya wanafunzi kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, ili wawe salama wakati wakiendelea na masomo yao.

“Leo ni siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika, ambapo sisi kama Shirika la Agape tukaona tuadhimishe kwa kutoa kifaa cha kisasa cha maji tiririka katika shule hii ya Msingi Lubaga, ili Juni 29 wanafunzi watakapofungua shule, waanze kukitumia na kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona,” amesema Myola.

“Naomba pia wadau ambao wanashughulika na masuala ya utetezi wa haki za watoto, walione suala hili kwa mapana na kwenda kutoa misaada ya vifaa hivi vya maji tirika mashuleni, ili kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya maambukizi haya ya virusi vya Corona,”ameongeza.

Naye Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Stella Lucas, amelipongeza Shirika hilo la Agape kwa kutoa msaada huo wa kifaa cha maji tiririka, huku akiomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia, ambapo bado wana uhitaji mkubwa huku shule hiyo ikiwa haina fedha za kutosha kununua vifaa hivyo.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Lubaga Lucas Venance, ameliomba Shirika hilo kuendelea kuchangia vifaa hivyo cha kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona mashuleni pamoja na wadau wengine, ikiwa kata hiyo ina shule mbili za msingi Lubaga na Azimio ambazo zote zina uhitaji mkubwa wa vifaa vya maji tirika ili wanafunzi wajikinge na Corona.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akizungumza katika shule ya msingi Lubaga mara baada ya kumaliza kukabidhi kifaa cha kisasa cha kunawa mikono na maji tiririka kwa wanafunzi shuleni hapo Juni 29 siku ya kufungua shule. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lubaga Stella Lucas, akitoa shukrani mara baada ya kumaliza kukabidhiwa kifaa cha kisasa cha kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na shirika la Agape.

Makamu mwenyekiti wa shule ya msingi Lubaga, Evarine Kaibale akitoa shukrani lwa shirika la Agape kwa kifaa hicho cha kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka.

Mtendaji wa Kata ya Lubaga Lucas Venance, akizungumza mara baada ya shirika la Agape kumalzia kukabidhi kifaa cha kisasa cha kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka katika shule ya msingi Lubaga.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, akitoa maelekezo namna ya kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka elimu ambayo watapewa wanafunzi Juni 29 siku ya kufungua shule, ili kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lubaga, Stella Lucas akinawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kwenye kifaa cha kisasa ambacho wamekabidhiwa na Shirika la Agape shuleni hapo.

Makamu mwenyekiti wa shule ya msingi Lubaga, Evarine Kaibale akinawa mikono kwa sabuni na majitiririka kwenye kifaa cha kisasa ambacho wamekabidhiwa na Shirika la Agape shuleni hapo.

Afisa mtendaji Kata ya Lubaga Lucas Venance, akinawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kwenye kifaa cha kisasa ambacho wamekabidhiwa na Shirika la Agape katika shuleni ya msingi Lubaga.

Mkurugenzi wa shirika la Agape John Myola, (aliyechuchumaa), akipiga picha ya pamoja, na walimu, mratibu elimu kata, na mtendaji, mara baada ya kumaliza kukabidhi kifaa cha kisasa cha kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka katika shule ya msingi Lubaga.


Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527