KAMANDA WA POLISI ATOA OFA KWA WALEVI SIKUKUU YA EID!!


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana, katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri, ametoa ofa kwa mtu yeyote atakayelewa kupita kiwango ahakikishe anawasiliana na Jeshi hilo, kwa ajili ya kulichukua gari lake na kulihifadhi na atapaswa kulifuata pale ulevi utakapomwisha.

Kamanda Shana ameyabainisha hayo, wakati akituma salamu za sikukuu hiyo na kuwataka wananchi wake kusherehekea kwa tahadhari, ikiwemo kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Natoa ofa pia kama ukijihisi umelewa kupita kiasi wewe tuite, tutachukua gari lako tutalitunza bure na kilevi chako kikiisha sisi tutakukabidhi, pia tunatoa wito kwa wananchi kuzingatia tahadhari zote za kujikinga na COVID-19" amesema Kamanda Shana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527