Wizara ya afya nchini Kenya imethibitisha maambukizi mapya 30 ya virusi vya corona hii ni baada ya sampuli 883 kufanyiwa vipimo katika muda wa saa 24 na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 465.
Naibu waziri wa afya Dk Rashid Aman anasema kuwa 19 ni wagonjwa kutoka Mombasa, 8 jijini Nairobi wawili kaunti ya Bungoma na kimoja kaunti ya Kitui.
Watu wawili zaidi aidha wamefariki kaunti ya Mombasa kutokana na virusi hivyo na kufikisha waliofariki nchini Kenya kuwa 24 na idha waliopona ni 167 baada ya watu 15 zaidi kuruhusiwa kuondoka hospitalini.