VIFO VYA CORONA NCHINI MAREKANI VYAKARIBIA LAKI MOJA, TRUMP AONEKANA AKICHEZA MCHEZO WA GOFU BILA BARAKOA


Vifo vya corona vinakaribia kufikia Laki moja Marekani ambapo hadi leo asubuhi kuna vifo 99,300, maambukizi pia yanaongezeka.


Marekani ina maambukizi 1,686,436 na wamepona Watu 451,702.

Rais Trump jana alionekana akicheza Gofu huku wakazi wa Marekani wakijianika juani wakati hatua za vizuizi zikianza kulegezwa nchini humo. 

Trump ambaye anataka makanisa, masinagogi na misikiti kuruhusiwa haraka kuendesha ibada, hakuwa amevaa barakoa wakati alipokuwa akicheza Gofu, na hata wachezaji wenzake nao hawakuvaa Barakoa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527