AFRIKA KUSINI KULEGEZA MASHARTI YA CORONA


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema maambukizi ya virusi vya Corona nchini mwake yanaendelea kuongezeka kama ilivyobashiriwa na wanasayansi.

Katikati mwa wiki iliyopita wanasayansi nchini Afrika Kusini walionya kuwa huenda watu 50,000 wakapoteza maisha na wengine zaidi ya Milioni tatu, kuambukizwa virusi vya Corona kufikia mwisho wa mwaka huu.

Wizara ya afya nchini humo iliwaajiri Wanasayansi hao kutoa taswira ya maambukizi hayo, na kubainika kuwa huenda kati ya watu 35,000 na 50,000 wakapoteza maisha kufikia mwezi Novemba.

Licha ya ongezeko hilo, kiongozi huyo amesema kuwa ifikapo tarehe 1 mwezi Juni, serikali itandoa masharti mengine ili maisha yaendelee kama kawaida.

Afrika Kusini kwa sasa ina visa vya maambukizi 22,583 baada ya visa vipya 1,240 kuthibitishwa. Wagonjwa 10,104 wamethibitishwa kupona ugonjwa wa Covid-19, ugonjwa ambao kufikia sasa umeua watu 429.

Raia wa nchi hiyo wametakiwa kuanza kuzoea kuishi na virusi hivyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527