VISA VYA CORONA VYAFIKIA 260 UGANDA, RAIS MUSEVENI KUGAWA BARAKOA BURE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 19, 2020

VISA VYA CORONA VYAFIKIA 260 UGANDA, RAIS MUSEVENI KUGAWA BARAKOA BURE

  Malunde       Tuesday, May 19, 2020

Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa serikali yake itatoa barakoa za bure kwa wananchi kuanzia miaka sita na kuendelea.

Akihutubia taifa Jumatatu,kiongozi huyo mwenye miaka 75 alisema ni lazima wananchi wote wavalie maski katika maeneo ya umma huku taifa hilo likijiandaa kurejesha uchukuzi wa umma kuanzia Juni.

Rais Yoweri Museveni alisema ni lazima Waganda wote wavalie maski kabla usafiri wa umma kurejeshwa.

“Maski hizi ni lazima zivaliwe kila wakati unatembea maeneo ya umma, endapo unapiga chafya, unazungumza ama kukohoa. Watu walilalamika  hawana uwezo wa kupata maski, serikali imeamua kutoa maski kwa kila Mganda kuanzia miaka sita na kuendelea," alisema Museveni.

Wizara ya Afya nchini humo imesema wagonjwa wengine 12 wa corona wameongezeka na kufanya idadi ya maambukizi kufikia 260, waliopona wamefikia 63 na hakuna kifo


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post