TRUMP ATISHIA KUIONDOA MAREKANI KWENYE SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO NA KUSITISHA MISAADA YOTE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 19, 2020

TRUMP ATISHIA KUIONDOA MAREKANI KWENYE SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO NA KUSITISHA MISAADA YOTE

  Malunde       Tuesday, May 19, 2020
Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuiondoa Marekani kwenye Shirika la Afya Duniani WHO, akidai kuwa taasisi hiyo ya kimataifa ni kikaragosi cha China.


Trump ametoa vitisho hivyo katika barua aliyomuandikia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia, Tedros Adhanom Gabrayesus ambapo amesema, "Marekani itaikatia misaada WHO kikamilifu iwapo haitapiga hatua kubwa za kujiboresha ndani ya siku 30 zijazo."

Rais huyo wa Marekani ametuma ujumbe uliouambatanisha na nakala ya barua hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika: Tunaipa WHO dola milioni 450 kila mwaka, lakini hawatutendei wema, wamekuwa wakitupa ushauri mbaya.


Hii ni katika hali ambayo, mwezi uliopita wa Aprili, Trump alitoa tuhuma kali  dhidi ya shirika hilo akidai kwamba linaipendelea China, na hivyo akachukua uamuzi wa kulitakia misaada ya kifedha.

Mbali na kuilaumu WHO, Trump pia amekuwa akidai kwamba China haikuweza kutoa kwa wakati muafaka taarifa za kuenea virusi vya corona wala kukabidhi takwimu sahihi za virusi hivyo kwa Shirika la Afya Duniani; ambapo pia alitishia kuwa huenda akaamua kukata uhusiano wa Washington na Beijing.

Hadi sasa Marekani ina visa 1,550,539 , vifo 91,985 na idadi ya wagonjwa waliopona ni 356,383


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post