SUDANI YAAMRIWA KUWALIPA FIDIA WAATHIRIKA WA SHABULIZI LA MABOMU UBALOZI WA MAREKANI KENYA NA TANZANIA LILILOFANYWA NA AL-QAEDA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, May 20, 2020

SUDANI YAAMRIWA KUWALIPA FIDIA WAATHIRIKA WA SHABULIZI LA MABOMU UBALOZI WA MAREKANI KENYA NA TANZANIA LILILOFANYWA NA AL-QAEDA

  Malunde       Wednesday, May 20, 2020

Mahakama Kuu nchini Marekani imeaiagiza  Sudani kuwalipa fidia waathiriwa wa shambulio la mwaka 1998 katika balozi za Marekani Nairobi nchini Kenya na Dar es salaam nchini Tanzania.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu nchini Marekani unawahusisha raia wa Marekani, wafanyakazi wa balozi hizo na wakandarasi.

Uamuzi huo unajiri wakati ambapo serikali ya Sudani inapigania kuondolewa katika orodha ya Marekani ya mataifa yanayofadhili ugaidi.

Uamuzi huo ulioungwa mkono na majaji wengi unamaanisha kwamba takriban Dola Milioni 800m kati ya Dola bilioni 4 ambazo ziliamrishwa na mahakama hiyo kuwafidia mwaka 2011 zimerejeshwa.

Mwaka 2017 , Sudan ilifanikiwa kuupinga uamuzi huo ikihoji kwamba walipatiwa fidia hiyo chini ya marekebisho ya sheria ya 2008 ambayo haiwezi kusimamia kitu kilichotokea miaka 20 iliopita.

Shambulio hilo la al-Qaeda kwenye balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania liligharimu maisha ya watu 224. Tangu mwaka 2001, karibu watu 600 wameendelea kuomba Sudan iwalipe fidia kwa sababu wakati huo Khartoum iliwapa hifadhi wanamgambo wa Kiislamu pamoja na Osama bin Laden.

Kesi hiyo ilifikishwa hadi Mahakama Kuu ambayo ilithibitisha kwamba Khartoum inapaswa kulipa fidia.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post