SPIKA NDUGAI ATOA MASHARTI YA KUMTIMUA BUNGENI CECIL MWAMBE


Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amewataka wale wote wanaotaka amfukuze Ubunge Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe, basi wamshauri amuandikie Spika barua ya kujiuzulu kwake, halafu waone kama ataendelea kukaa bungeni.

Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 12, 2020 na kusema kuwa maamuzi hayo yote ya kumrejesha Mwambe bungeni, yamekuja kutokana na yeye kupata barua ya upande mmoja.

"Nimeeleza Mwambe amewahi kuniandikia barua lini?, hivi wewe ungekuwa Spika ungefanyaje, huna barua ya mtu kujiuzlu ungefanyaje?, unamfukuza tu!, lazima mchunguze na muangalie mzani uko wapi, Mwambe yupo hajafa, mwambieni aandike barua anikabidhi mimi, akishanikabidhi muone kesho yake itakuwaje" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai amesema kuwa leo jioni atatolea ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na CHADEMA, kwamba Wabunge wake waliojiweka karantini kwa sasa hawatorudisha posho kwa sababu wao siyo wezi


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527