SERIKALI YASISITIZA KUTOA USHIRIKIANO KWA WASANII

Adeladius Makwega -WHUSM

Serikali imesisitiza kuendelea kutoa ushirikiano kwa wasanii kupitia vyombo na idara zake zinazosimamia sekta hiyo ili kusaidia kazi zao kufahamika zaidi ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipotembelewa na msanii Ezekiel Mwakipageme maarufu kama Sud Black ambaye ni msanii wa sanaa ya maigizo.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa sanaa ya Tanzania inapofanyika sehemu yoyote ni vizuri kuwa ya mfano na yenye motisha kwa wale wanaotaka kufanya kazi za sanaa pamoja na wale wanaozifuatilia kazi hizo.

“Hongera kwa kucheza picha nyingi, kuigiza na wasanii wengi wakubwa na kwa kufanya hivyo umeweza kuibeba na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini China na kimataifa.” Amesema Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wake, msanii Ezekiel Mwakipageme amesema kuwa anatarajia kuwakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza katika ulimwengu wa filamu kwa kujenga studio ya kisasa, chuo cha michezo na pia kufungua miradi mingine ya maendeleo ikiwemo huduma za afya.

“Nimecheza filamu nyingi na wasanii wakubwa kama Jack Chain na wengine na hivi karibuni zitatoka filamu zangu mpya mbili, Watanzania watarajie mengi makubwa katika tasnia hii ya filamu”, Alisema msanii Sud Black.

Nae Mtayarishaji wa Filamu, John Kalage ambaye ndiye Mkurugenzi wa msanii huyo hapa nchini Tanzania ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaoutoa katika masuala yote ya Filamu na Sanaa. kufanya kazi zetu kwa kufuata miongozo yote ya serikali na kuondoa migongano isiyo ya lazima”, Amesema Mkurugenzi Kalage.

Serikali ya Awamu ya Tano kama ilivyotoa ahadi yake ya kukuza sanaa na wasanii kwa kufanya kazi za sanaa kuwa ajira kwa vijana imeendelea kutekeleza ipasavyo huku baadhi ya wasanii wakiendelea kuibuka na kazi zao kuvuka mipaka ya taifa letu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527