RC MAKONDA AWATAKA WALIOFUNGA BAA, MAHOTELI KISA CORONA WAFUNGUE WACHAPE KAZI.....WALIOKIMBILIA MIKOANI PIA WARUDI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 19, 2020

RC MAKONDA AWATAKA WALIOFUNGA BAA, MAHOTELI KISA CORONA WAFUNGUE WACHAPE KAZI.....WALIOKIMBILIA MIKOANI PIA WARUDI

  Malunde       Tuesday, May 19, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Watu wote waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waendelee kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.

RC Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

Aidha RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo.

“Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea.

"Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwahiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida” Amesema RC Makonda


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post