MWANDISHI WA HABARI AJIUA KWENYE MTIMwandishi wa Habari wa kituo cha runinga cha K24 nchini Kenya amejitoa uhai kwa kujitia kitanzi katika kaunti ya Nakuru.

George Kori alitoweka Jumanne, Mei 19,2020 na amekuwa akitafutwa na wenzake bila mafanikio. 

Amepatikana leo Jumapili, Mei 24, katika eneo la Gatura wadi ya Elburgon akiwa amejitia kitanzi. 

"Mwili wake umepatikana ukining'inia juu ya mti," amesema David Kamau aliyeshuhudia.

Bado haijabainika ni kwa nini Kori aliamua kujitoa uhai.

Via Tuko

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527